Hata ya Mkopo Hakuna! Baba Diamond Azungumzia Kutonunuliwa Gari Na Mwanaye

Baba Diamond Azungumzia Zawadi Ya gari

By  | Nov 20, 2020, 12:35 PM  | Diamond Platnumz  | Drama

Baba mzazi wa msanii  Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka kuhusu ishu ya yeye kutozawadiwa gari na mwanawe licha ya kuwa Diamond amekua akiwapa watu wengu magari.

Akizungumza katika mahojiano na Ipo TV Mzee Abdul amesema watu wamekua sio waelewa juu ya mambo yanayofanyika.

Amesema, Diamond ana jina kubwa na anaweza akamchukulia gari mtu kama Zuchu sababu ni mtu wa karibu yake na anamfanyia kazi, hivyo anaweza kumchukulia gari kama udhamini tu.

“Ile inaweza ikawa kama udhamini akawa anapata kipato akamlipia kidogo kidogo, ni jambo la kawaida, kama mkopo wa kitu Fulani. Anaweza akamuita ghafla kwa hiyo anahitaji kuwa na usafiri”. Alisema Babab Diamond.

Aliongeza kuwa, suala la gari kwake ni la kawaida kwani alishawahi kumiliki hata Kabla ya Diamond kumiliki.

Mzee Abdul ameongeza kuwa, anashukuru kuna mahitaji anamtimizia, na hivyo vitu vingine ni vitu vya kawaida tu.
Youtube embed
Read more