Mji wa moto huu! Daily mastory mapya tu! Linalomalizia kutrend kwenye mitandao kama moto wa nyika ni juu ya uraia wa mwanamuziki Nasibu Abdul alimaarufu kama Diamond Platnumz kama ni Mganda au Mtanzania. Cheki hii coment hapa kwenye moja ya post katika ukurasa wa Carrymastory irenekhanthiopy
Kumbe Diamond Sio Mtanzania! Baba mzazi wa msanii Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka na kusema kwamba Diamond sio Mtanzania ila ameegemea sana kwa upande wa mama na kujiita mkigoma.
Akielezea uhusiano wa Diamond na Ukigoma katika mahojiano na Ipo TV Mzee Abdul amefunguka na kusema kuwa Diamond alizaliwa Hospitali ya Amana Dr es Salaam mwaka 89, akaishi Kariakoo na baadae akaenda Tandale.
βKutokana na Nasibu kubase sana upande wa Mama, ndomana anajiita mtu wa Kigoma lakini kwa kufuata sheria ilivyo, Nasibu ni Mganda sio mtu wa kigoma sababu mimi baba yake baba yangu ni Mganda mama ni Mnyirambaβ. Alisema Baba diamond.
Mzee Abdul ameongeza kuwa, anaimani nasibu kujiita mtu wa Kigoma mara ya kwanza alienda alivyoimba nyimbo ya Kigoma na dada yake Queen Darleen na mara ya pili alivyoenda kwenye Tamasha lake lakini sio mtu aliyezaliwa Kigoma, amezaliwa Dar es Salaam.
Mzee Abdul ameongeza kuwa, Diamond anaweza akachagua popote anapopenda kuegemea kama ni Kigoma au Uganda.