Dullah Afunguka Ishu Ya Diamond na Kiba

Dullah afunguka kumpendelea Kiba

By  | Nov 20, 2020, 12:35 PM  | Diamond Platnumz  | Drama

Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV na EA Radio Dulla amefunguka kuhusu uvumi ulioenea wa yeye kumpendelea Alikiba kuliko Diamond.

Akizungumza kuhusu shutuma hizo wakati wa Mahojiano na Salama katika kipindi cha Yah Stone Town Dullah alisema wasanii wote wawili yaani Diamond na Kiba ni mararafiki zake na amefanya nao kazi.

“Diamond tumefanya nae kazi tangu akiwa mchanga sana na kama unavyojua planet Bongo nimeishi nayo miaka mingi sana na tumepambana nae miaka yote, hiyo ni sawa kwa upande wa Ally pia na uzuri yeye alikuwepo hata kabla ya mimi kuanza utangazaji. ” Alisema Dullah.

“Tatizo lilikuja sehemu moja, kuna wakati ilitokea sintofahamu kutokana na kutokuenda sawa kibiashara kati ya kampuni nnayofanyia kazi na wasanii na mimi ni muajiriwa. Hiyo ikapelekea ukaribu wangu na Nasibu kupungua sababu hatufanyi kazi wala kupigiana simu za interview lakini Ally anafanya kazi na kampuni yangu so lazima nitafanya nae kazi.” Aliongeza Dullah


Aifafanua kuwa, kutokana na kuonekana sana na Ally kwakua tu anafanya nae sana kazi kumezua maneno lakini hiyo sio ishu binafsi bali hali iko hivyo kutokana na ajira yake.

Youtube embed
Read more