Harmonize amatambulisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuwa mlezi wa lebo ya Kondegang

Day 2 meeting na mlezi wetu

By  | Nov 20, 2020, 12:37 PM  | Harmonize  | Drama

Post main image
MSANII wa Bongo Fleva, Adul Rajabu marufu kama Harmonize, amemtambulisha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kama mlezi mpya wa lebo ya Kondegang.
Harmonize amemshukuru Rais John Magufuli, kumteua Kunenge, kwa sababu amekuwa mlezi na msimamizi wa usalama na maendeleo ya vijana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram leo, Harmonize ameandika kuwa,    “Kipekee kabisa ningependa kumshukuru Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli, kwa kututeulia RC @abubakar_kunenge aendeleze pale walipoishia viongozi wetu wengine watukufu walio pita, katika harakati za kuikuza na kuing’arisha Dar es Salaam.
“Tunaamini Dar es Salaam ni Jiji kubwa na lenye dhamana kubwa mipango mingi ya maendeleo,” ameeleza msanii huyo mashuhuri nchini.
“Nitakuwa sijakosea sanaa nikisema ndio sura ya Taifa hili. Achilia mbali shughuli nyingi za kiutendaji sambamba na hilo kuna akina sisi vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa bila kupepesa macho tunahitaji mtu wa kutuongoza, kutusimamia, kututetea na kuturekebisha pale tunapoteleza ili tuweze yafikia malengo yetu ya kuzisaidia familia zetu maskini.”
“Itoshe tu kusema tumepata mlezi na msimamizi wa usalama pamoja na maendeleo yetu …!!!! @abubakar_kunenge KAZI ZIENDELEE…!!!!! Wana Dar es Salaam tujivunie…!!! 🙏 Day 2 Meeting na mlezi wetu @kondegang New Dar es Salaam.
 
 
Read more