Mambo Ni Moto! Mkubwa asema Diamond Atabaki Kuwa Juu ya Harmonize

Mwalimu Hawezi Kuzidiwa Na Mwanafunzi

By  | Nov 20, 2020, 12:34 PM  | Harmonize  | Drama

Unaambiwa mambo ni moto, mambo ni firee baada ya Baba wa Msanii Diamond, Mzee Abdul kuzungumzia suala la Harmonize kutoka katika Lebo ya WCB na kuanzisha lebo yake Konde Gang.

Akizungumza na Ipo Tv Online Mzee Abdul amesema kuwa, suala la kuondoka Harmonize WCB ni kama vile Timu ya Simba, ukimtoa huyu atakuja mwingine kwani wapo wenye ujuzi wengi.

Ameongeza kuwa, anampongeza Harmonize kwa suala la kutoka WCB cha muhimu tu hamdharau Diamond.

“Naimani hata vitu vingine Harmonize anavyofanya anafuata nyendo za alipotoka, hakuna matusi wanayotukanana, kajiweka peke yake na mimi namuombea Mungu aweze zaidi, apate kipato na apeperushe bendera ya Tanzania’ Alisema Baba Diamond.

Ameongeza kuwa hivyo ndivyo inavotakiwa sio kung’ang’ania kukaa sehemu moja na kushindwa kutambua kitu unachikifanya.

Amesema, ana imani hakuna mtu anayemtukana mwalimu wake hata siku moja na hakuna mwalimu anayezidiwa na mwanafunzi wake hivyo Harmonize hawezi kumzidi Diamond Mia kwa mia.

“Mwalimu atabaki kuwa mwalimu na mwanafunzi atabaki kuwa mwanafunzi, labda ziada tu ya pembeni inatokea baadae  na hata kama atamzidi kuna muongozo Fulani lazima apate kwa mwalimu wake” Alisema mzee Abdul.

Kuhusu kumpendelea Diamond Mzee abdul amesema hakuna kitu kama hicho ila ukweli ndo ulivyo mwalimu atabaki kuwa mwalimu.

Na suala la Kiba kusahaulika kisa bifu la mashabiki wa Diamond na Harmonize Mzee Abdul amesema kuwa, Kiba hajasahaulika na kila mmoja ana mashabiki wake.

Youtube embed
Read more