'Ushamba' Wa Harmonize Wawatoa Povu Mashabiki!

Mashabiki Wamtolea Povu Harmonize

By  | Nov 20, 2020, 12:33 PM  | Harmonize  | Drama

Post main image
Msanii wa Bongo Fleva mwenye lebo yake hapa mjini, Harmonize amewatoa  povu mashabiki kutokana na ‘Ushamba’

Kutokana na post za Harmonize katika ukurasa wake wa Instagram, inaashiria kwamba kuna kibao anatarajia kukiachia kitakachokwenda kwa jina la ushamba.

Baadhi ya posti zimekua zikibeba mistari ambayo mashabiki wake wanaamini inatoka katika nyimbo hiyo ambayo wengi wanaishubiria kwa hamu huku wengine kama kawaida ya mashabiki, wakitoa povu(Malalamiko)

Yupo shabiki aliyehoji kama nyimbo hiyo itaweza kurudisha wabunge wa upinzani, na kuongeza kwamba ana stress na matokeo akiashiria kwamba katika kipindi hiki cha matokeo ya uchaguzi haitaji kusikia habari za nyimbo.
View this post on Instagram

STAY CONECTED 🏁1/11/2020 🐘

A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on

Shabiki mwingine alimtolea Povu Harmonize kwa kudai kwamba anamkubali sana ila haelewi kwa nini nabishana na aliemtoa kimaisha na kumwambia yeye ndo mshamba. Povu la shabiki huyu linaashiria kwamba hisia zake zinamuaminisha kwamba kibao hicho cha Ushamba kinaweza kumuhusu 
Shabiki mwingine aliandika kwamba ni vita gani hiyo ya upande mmoja wakati upande mwingine hawana muda, akimaanisha hao anawaimba hawana muda na vita ya maneno huku shabiki mwingine akimwambia kwa sasa upepo wote uko kwenye siasa hivyo akimaanisha sasa si muda sahihi wa kutangaza nyimbo.

Kwa upande mwingine, wapo mashabiki walomsifia na kumwambia wananogoja kwa hamu wimbo huyo, Shabiki mmoja alimwambia anangoja wimbo huo afanye cover huku wengine wakimuomba asiachie wimbo huo mpaka mtandao utakapokuwa sawa kutokana na network kusua sua kipindi hiki cha uchaguzi.

Pitia maoni ya mashabiki hapa chini upate kuoana povu la baadhi ya mashabiki huku wengine wakimsifia;
image.png 39.48 KB
image.png 40.34 KB
image.png 34.79 KB
image.png 34.96 KB
image.png 41.61 KB


Read more