Katika ukurasa wake wa Instagram Jokate amesema, "Nitumie fursa hii pia kuwashukuru wanakijiji cha Zegero kwa kutoa eneo hili kwa jeshi letu la polisi."
"Mipango ya hivi karibuni ni kujenga chuo cha mafunzo ya kikosi cha askari polisi kwenye kijiji chetu," amesema Mkuu huyo wa wilaya.
Amesema amemhakikishia Kamanda wa Kikosi hicho, ushirikiano wote utakaohitajika kutoka kwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya.