Kiki Bongo Unatoboa, Kenya Unakufa

Kiki na Muziki

By  | Nov 20, 2020, 12:35 PM  | Drama

Nyota wa muziki kutoka Kenya ambaye anafanya vizuri sana kwenye game la muziki nchini humo na Afrika Mashariki kwa ujumla, msanii Nadia ameeleza namna ‘kiki’ zinavyochukuliwa kwa upande wa nchini Kenya.

Akizungumza jana kupitia CloudsFm, hitmaker huyo wa ngoma ya ‘wangu’  alisema, “Kwa Tanzania kiki inampandisha msanii, ila hilo liko tofauti sana kwa Kenya, Kiki inakushusha kwa haraka kuliko kukupandisha.
Nadia


Ukifanya kiki Kenya uwe makini sana, kwani muziki wa Kenya na mashabiki zake umejengwa katika misingi ya kuamini katika heshima ya nchi na kipaji cha msanii kuliko kiki” alieleza Nadia
Nadia & Marioo


Nadia ambae amewahi kushirikiana kimuziki na msanii Mario wa hapa nchini aliweka wazi pia mahaba yake kwa msanii Maua Sama akimsifia kuwa ni msanii mwenye kipaji kisichofichika na ambae hatumii kiki kama sehemu ya kumfikisha mbali...

“Namkubali sana, sana, sana Maua Sama, ni msanii ambae anafanya kazi kwa bidii sana, na ambae kipaji chake hakifichiki, nampenda sana”
Read more