Mahaba Ya Hamisa Mobetto, Otile Brown Gumzo Mitandaoni

Hamisa Na Otile Brown Wazua gumzo

By  | Nov 20, 2020, 12:35 PM  | Drama

Bongo hakuishi vimbwanga, kila siku yanazuka mapya na leo ni video inayozagaa mtandaoni ikimuonyesha Msanii wa Bongo Fleva  Hamisa Mobetto akiwa pamoja na Msanii wa muziki kutoka Kenya Otile Brown.

Picha hiyo imezua gumzo kutokana na mashabiki kutabiri ukaribu uloonekana katika video hiyo kuwa huenda yakawa ni mahusiano au ni video mpya.

Kwa sasa, Hamisa anatamba na kibao cha ‘Ginger Me’ ambacho hakina muda sana tangu kuachiwa kwake na hajathibitisha hadharani kuwa katika mahusiano.

Video hiyo inayozagaa haikuwaacha wabongo nyuma kwani wapo walotoa povu haswaa huku wengine wakitabiri kuwa ni kiki ya ujio wa nyimbo mpya.


Soma Comment hapa chini upate kujua maoni ya Wabongo na mashabiki wa Hamisa kwa ujumla;
Youtube embed


Read more