Shamsa Awafunda Mashabiki

Shamsa Awaasa Mashabiki

By  | Nov 20, 2020, 12:35 PM  | Shamsa Ford  | Drama

Muigizaji wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amewafunda mashabiki zake kuhusu kushinda katika maisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa ameandika  “Hakuna kitu kizuri kwenye maisha kama kushinda haijalishi kwenye upande upi ila ushinde tu.pambana na ushinde kwenye unachokipigania”.

Mbali na hilo, katika posti nyingine shamsa amewaasa mashabiki wake waishi maisha yao na wayafurahie kwani mwisho wa siku hakuna anayetoka hai katika maisha haya.

Shamsa, amekuwa akitupia picha zenye caption ‘jumbe’ zenye mafunzo mbali mbali na busara kubwa ndani yake ambazo mashabiki zake wamekua wakizifurahia.

Hizi hapa ni baadhi ya jumbe za Shamsa kutoka katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram;
jichunguze ww una tabia gani kabla ya kumsema mwenzio.Hata kwenye ndoa kabla ya kumsema mumeo tabia yake kwanza jichunguze ww mapungufu yako inawezekana tabia yako ndo inayomfanya Mumeo awe na tabia mbaya zaidi .Mtu huwa ni ngumu kuona mapungufu yake zaidi ya watu ambao wapo karibu yako ndo wataona mapungufu yako.

Kulia ni tiba na kuongea ni tiba ukijisikia kulia lia sana na ukijisikia kuongea onge sana ila angalia unaongea kwa kina nani.

Kinachokuumiza wewe usimfanyie mwenzio maumivu atayoyasikia yeye na ww ni hayohayo.
 Karibuni sana

Muda mwingine pesa ni kila kitu na muda mwingine
pesa si kila kitu .kuna muda unahitaji vitu ambavyo hata pesa haiwezi kununua kama upendo na amani.kuna muda unatamani uzungukwe na watu wanaokupenda kwa dhati hata kama una pesa huwezi kupata upendo wa kweli labda wataoipenda pesa yako .Pesa hainunui kila kitu

Mungu anapokusogeza mbele kimaendeleo pia kumbuka viwango vya maadui vinaongezeka. usiache kumuomba MUNGU kila wakati akulinde na maadui unaowajua na usiowajua


Anayekupenda hatokuumiza labda kwa bahati mbaya kwasababu hakuna binadamu aliyekamilika

Read more