Tommy Flavour Afunguka ya Officialllyn

Tunasikilizana

By  | Nov 20, 2020, 12:35 PM  | Drama

Nyota mpya wa Bongo Flava, msanii Tommy Flavour amefunguka kuhusu mapenzi yake na mrembo Irene maarufu Officiallyyn


Akizungumza jana na kipindi cha Dadaz kinachoruka EATV amesema mahusiano yao yamefanikiwa kutokana na utulivu wao toka walipoanza miezi saba iliyopita.


“Mimi nipo na Official Lyyn, sasa hivi tuna muda wa miezi saba tangu tumekuwa pamoja, ishu ya kwanza ilikuwa ni utayari na u-serious hivyo ndiyo vitu vinavyofanya mahusiano yetu kuwa na nguvu” amesema Tommy Flavour.

Hit maker huyo wa 'Omukwano' Kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la The One.
Youtube embed
Read more