Uchebe amrushia kombora Shilole amuita "nuksi'

Asema milango yake imeanza kufunguka

By  | Nov 20, 2020, 12:36 PM  | Drama

Post main image
Ashrafu Sadick maarufu kwa jina la Uchebe amerusha kijembe kwa Mwanamuziki Zuena Mohammed maarufu kwa jina la Shilole akidai kuachana naye milango yake imeanza kufunguka.

Julai 8 mwaka huu Shilole alitangaza kuvunja ndoa yake na Uchebe kwa kile alichodai kupigwa mara kwa mara na mume wake na kuweka picha alizoumizwa katika mitandao ya kijamii.

Jana usiku kwenye akaunti ya Instagram ya Uchebe aliandika ujumbe huu "Kuna watu wakiondoka kwenye maisha yako mlango huanza kufunguka,
Tajiri kwa huu mchongo dah atakulipa Mungu,"


Baadhi ya mashabika katika ukurasa huo wa Instagram wamemponda vikali Uchebe kwa kauli aliyoitoa  huku wakimuambia amshukuru Shilole aliyemfanya ajulikane.

Mwingine aliandika ujumbe huo inaonyesha kuachwa na Shisi  umeumia sana sio kwa vijembe hivyo.

"Wanaume jamani ila Shisi alisema tumpe muda tutaijua tabia yako aisee wewe ni wa ovyo," aliandika Sophia-mkumbo.

"Haa wewe hebu kua mwanaume mwishowe tukuvalishe vijora maana umekuwa shambenga kama Khadija Yusuph khaa yaani Shisi ndio kapewa roho ya kiume na wewe umekuwa mwanamke kutwa vijembe  ovyo.. jaribu kuishinda nafsi unajiita mwanaume alafu kutwa vijembe hebu tulia,"

"Mtu hakuzuii kupata riziki. Ni muda sahihi ulikuwa haujafika,"

"Daa unazingua sana we mwanaume au mfano wa mwanaume huyu Shishi unayemuona alikuzibia milango usingewajua hao kina vunja bei, ungewajulia wapi,"


Read more