JayDee awashukuru mashabiki asema bado story saba

JayDee kuanza kuanika story alizopatiwa

By  | Nov 20, 2020, 12:37 PM 

Post main image
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura, maarufu kwa jina la Lady JayDee amewashukuru mashabiki wake waliomuandikia habari na kukubali kushiriki naye siku ya Desemba 5, 2020.

Jaydee ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Instagram huku akieleza kuwa bado atapokea story nyingine saba zitakazokidhi mahitaji yao ya Backstage.

“Wiki hii nitarusha story ya kwanza kabisa ili mpate kuelewa mlengo wa kile tunachokitazamia,” aliandika Jaydee.

Aliongezea kuwa “Usiache ku subscribe kwenye you tube channel yangu kupitia link kwenye bio #20 Albumlaunch#20yearsofladyjayDee#backstage#backstageatladyJayDee#LadyJayDeeBackStage,”

https://www.instagram.com/p/CGhstIKJKhY/?igshid=4iev1tkp18gc

Msanii huyo anatarajia kukaa meza moja na mashabiki zake katika uzinduzi wa albamu yake ya 20 itakayozinduliwa Desemba 5, mwaka huu.

Mashabaki hao 20 ni wale ambao wenye historia ya nyimbo zake zinazotoka walikuwa wapi, wanafanya nini na kipi kilichowagusa.

Katika story 20 bora za mashabaki wake atakazozikubali atarekodi na kushare nao kwenye majukwaa mbalimbali.

“Natafuta story 20 zitakazovutia na watu hao watakaa na mimi backstage siku ya uzinduzi wa albamu yangu ya 20 na tutapiga story uso kwa uso,” alieleza JayDee kupitia mtandao wa kijamii.

Read more