JayDee awajibu Basata baada ya kufungia wimbo wake

Basata yafungia wimbo wa JayDee

By  | Nov 20, 2020, 12:43 PM  | Lady Jaydee 

Post main image
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limefungia wimbo wa  Msanii wa Muziki wa bongo Fleva, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jayde kwa  kosa la kuhamasisha vitu visivyokuwa  na maadili nchini.

Wimbo huo uliofungiwa unaitwa 'one time' inasemekana ule mstari alioimba tu smoke weed japo one time'

Meneja wa msanii huyo, Mx Carter  amesema leo wamepokea barua rasmi ya kufungiwa kwa wimbo  huo.

Alisema waliitwa na Basata wakajulishwa kuna vitu ambavyo havijakaa sawa na walikwenda na kupatiwa barua.

"Kuna mstari ambao nisingependa kuujtaja ambao wamesema unahamasisha vitu ambayo sio vya kimaadili ya kitanzania," alisema.

Muda mfupi baada ya kufungiwa kwa nyimbo yake Jaydee katika akaunti yake ya Twitter aliandika ujumbe huu akiwa ameweka picha ya chakula "Hatuwezi kuacha kula kwa ajili ya mambo madogo madogo,"

Baadhi ya mashabiki katika ukurasa huo walimuambia kuwa ana nyimbo zaidi ya 100 kufungiwa nyimbo moja haitawasaidia.

"Hata wakufungie kufanya muziki, hakuna kuimba kwenye kampeni zao," aliandika Jenipher Joseph.

"Ndiooooo najua umepita pazito watu kadhaa hawawezi kukutikisa usifanye yako,"

Shabiki mwingine aliandika ujumbe huu"Kula muhimu sn wamefungiwa wangapi na maisha yanaenda mpaka tunafika Nyegezi freshi kabisa,"
Read more