Wolper kadata na penzi la mwanamitindo mwingine

Acha nionekane chizi wa mapenzi

By  | Nov 20, 2020, 12:37 PM  | Jacqueline Wolper  | Relationships

Post main image
MALKIA wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper Massawe, amesema kuwa, amekufa ameoza kwenye penzi jipya la Rich Mitindo.

Wolper ambaye pia ni mwana mitindo amesema yupo tayari aonekane chizi, kwa kudata kwenye penzi hilo jipya.
 
Wolper amenukuliwa na IJUMAA SHOWBIZ akieleza kuwa, watu wengi wanamuona kama chizi kwenye penzi hilo, kwani amejitosa moja kwa moja huku akiwa haambiliki wala hasikii la mtu.
 
“Acha waniite chizi, lakini ukweli ni kwamba, sasa hivi nimenasa kwenye huba la kweli nililolitafuta siku nyingi sana na sikuwahi kulipata,” amesema Wolper.

Kabla ya kuzama kwenye penzi hilo Jipya, miezi minne iliyopita Wolper aliwahi kuzama kwenye penzi la mwanamitindo mwingine Chidi ambaye licha ya kumvalisha pete ya uchumba hawakudumu.Read more