Rayvanny Out WCB? Na Mambo 9 ya Daimond Platnumz

Rayvanny Kufungua Lebo

By  | Nov 20, 2020, 12:33 PM 

Post main image
 Nyota wa muziki nchini, msanii Diamond Platnumz jana kupitia kipindi cha The Switch cha Wasafi FM amefunguka mambo mengine exclusive kuhusiana na muziki wake, biashara, na mahusino. Huu hapa ni mkusanyiko wa yale makubwa aliyoyaongea jana.
 MOJA
''Nyuma kidogo kabla sijaanza kuimba nilikuwa na-rap. Hata kabla ya kuanza kufanya muziki pia nilikuwa Dancer, nilikuwa nashuti sana Video za wasanii kama Dancer''

MBILI

''Sio Kweli kwamba wasanii wanaingiza pesa Youtube, maana kwa ninavyojua mimi ukipata Views Million moja... Unapata kama Millioni moja au Laki tisa hivi, lakini ukitapa Stream au Downloads Millioni moja ni zaidi ya Billion 2. Watu wanatakiwa kuzingatia sana Itunes''

TATU
''Ukitaka sanaa ikue lazima kuwe na Ushindani, ukisema Simba na Yanga wapatane basi na Mpira imekufa hapo hapo. So ili Muziki ukue lazima mambo hayo yawepo lakini kwa Uchanya sio ifike hadi kwa Familia''

NNE
''Naomba wawekezekaji waongezeke kwenye Sanaa. Serikali imeshaifanya Sanaa kama sekta rasmi. Kama wanavyoweza luwekeza kwenye vitu vingine basi waongezeke kwenye Muziki pia. Wasafi peke yake haiwezi kuwashika wasanii wote''

TANO
''Na hapa hivi karibuni Rayvanny atafungua Label yake pia. Na kama akipost Studio yake basi itakuwa mdio Studio nzuri zaidi Tanzania mzima''

SITA
''Ntajiona mjinga sana siku nikifulia na itakuwa kumkosea hata Mwenyezi Mungu pia maana ataona kama alinipa mtu ambae sio, Lakini siwezi kubaki kwenye Muziki tu''

SABA
''Mama alipata Strock kabla Tiffah hajazaliwa. Nilichanganyikiwa sana. Gharama nilizotumia haikuwa rahisi. Alienda India mwezi mzima. Gharama nilizotoa lipindi kile kama nisingekuwa Mwanamuziki sijui ingekuwaje. Namshukuru sana Kusaga alinilipia Tiketi ya Ndege. Na aliporudi Ilikuwa kila siku matumia Millioni''

NANE
"Nilisema Nataka kufanya muziki uonekane na thamani, hivyo najitahidi kuwekeza na kuwapa riziki vijana wa mtaani. Nipo kwenye hatua za mwisho za Kiserikali na hivi karibuni ntafungua "Wasafi Betting", Kila kitu kipo tayari "

TISA
''Inshallah tuombe Heri, mambo ya Ndoa anapanga Mungu maana hapa Town ndele nyingi, unaweza kutangaza Ndoa hapa ni hatari''
Read more