Wema asalimu amri Instagram

asema wanajua kuzusha maneno

By  | Nov 20, 2020, 12:36 PM 

Post main image

Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu amenyoosha mikono juu kwa mtando wa kijamii wa Instagram akidai mashabiki wanajua kutengeneza baadhi ya mambo.

Wema aliandika ujumbe huu katika mtandao huo “Ila Insta kwa kutengeneza mambo [email protected],”.

Msanii huyo alitupia video yake ya tangazo la Cook with Wema Sepetu akiongea na Kajala Masanja kuhusiana alivyofananishwa mtoto wake Paula na Sonia.

“Walikuwa wanatengeza vitu ili watu wagombane Sonia aliakuwa ni rafiki wa Paula na Sonia akiwa likizo alikuwa anakuja nyumbani na hata Chrismass tunatoka pamoja,”alisema Kajala.

“Huwezi kufananisha akili za mtu na mtu Wema una akila yako na mimi nina akili yangu huwezi kulazimisha Sonia akifaulu basi na Paula afaulu hapana,”

Shabiki katika ukurasa huo anayejiita bint wa said alisema Insta weka kichwa cha habari tu.. habari kamili watamalizia.

Fatty ser aliandika ujumbe huu “Maskini… mahakimu wa insta wamezidi,”.

Read more